Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky amesema kwamba Urusi inatakiwa kuadhibiwa kwa kuivamia nchi yake.

Ameliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa huko New York kupitia video iliyorekodiwa kwamba uchunguzi wa uhalifu wa kivita unatakiwa kufanyika nchini humo. 

Pia ameongeza kwamba amekuja na mipango mingine ya kuendeleza mapambano na Urusi ikiwemo kuwekeza zadi kwenye jeshi .

Rais Putin  wa urusi hapo awali aliweka mipango yake ya kuwaita askari wastaafu wa zamani takribani laki tatu kuingia vitani kuendeleza mapambano .Tamko hilo limezua maandamano ambayo Bwana  Zelensky amesema kuwa ni kiashiria cha adui yake kutokua tayari kwa mazungumzo ya amani.