Jumanne , 28th Jun , 2022

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kukwete (JKCI) imekuja na teknolojia mpya ambayo inamfanyia upasuaji mgonjwa wa moyo bila ya kumuongezea damu kama ilivyokuwa inafanyika awali. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi,

Akizungumza na EATV Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi, amesema teknolojia hiyo ambayo tayari wameanza kuitumia kwa wagonjwa itamaliza changamoto ya kukosekana Kwa damu zilizokuwa zinahitajika kwa wagonjwa kabla ya kuwafanyia upasuaji huo.