Kamishna Uhamiaji na Udhibiti wa Mipaka Samweli Miharane
Kamishna Uhamiaji na Udhibiti wa Mipaka Samweli Miharane, amesema mtu huyo alikuwepo nchini akitumia hati ya kusafiria inayomruhusu kuingia na kuishi nchini Tanzania kwa muda mrefu inayofahamika kama Multiple Visa ambayo amekuwa akisaidiwa na baadhi ya Watanzania kupata nyaraka hizo za kuishi hapa nchini
Aidha Kamishna Miharane amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu kumekuwepo na wimbi kubwa la kuingia kwa wahamiaji haramu hapa nchini ambapo wahamiaji 18,289 walikamatwa huku mikoa ya Pwani na Tanga ikiongoza kwa kuingia wahamiaji hao
Katika hatua nyingine Kamishna Miharane amewataka Watanzania kuacha kuwasaidia wahamiaji haramu kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa nchi na watanzania kwa ujumla.