Uchumi wa dunia kukua kwa 2.7% mwaka 2017

Wednesday , 11th Jan , 2017

Uchumi wa dunia kwa mwaka huu wa 2017 unatarajiwa kukua kwa wastani wa asilimia 2.7 baada ya mdororo mkubwa mwaka jana.

 

Hiyo ni kwa mujibu wa benki ya dunia, katika taarifa yake ya jana ikisema vichocheo ni kupungua kwa vikwazo vya soko na kuendelea kwa biashara za nje huku mahitaji ya soko la ndani yakiendelea kuongezeka.

Taarifa hiyo inasema kuwa nchi kama Marekani, sera za kifedha zinatarajiwa kuchagiza ukuaji kwa asilimia 1.8 ingawa ongezeko la vikwazo vya kibiashara linaweza kuwa na athari hasi katika ukuaji huo.

Kwa upande wa nchi zinazoibuka kiuchumi, ukuaji unapaswa kuongezeka hadi asilimia 4.2 mwaka huu kutoka asilimia 3.4 mwaka uliotangulia kutokana na ongezeko la bei za bidhaa.