Uchaguzi kufanyika 2019

Wednesday , 11th Oct , 2017

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, imesema uchaguzi mkuu nchini humo sasa utafanyika Aprili mwaka 2019, hatua ambayo huenda ikazua vurugu miongoni mwa wapinzani.

Awali uchaguzi mkuu nchini humo ulipangwa kufanyika Novemba 2016, lakini Tume ya Uchaguzi ikadai haina uwezo kuandaa uchaguzi huo. Wapinzani wa Rais Joseph Kabila wanamtuhumu kwa kuchelewesha uchaguzi ili aendelee kubakia madarakani.

Kushindwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu Novemba 2016 kulizua maandamno ya kumping Rais kabila jijini Kinshasa ambapo mamia ya watu waliuwawa na wana usalama walipojaribu kuzuia maandamano hayo.