''Tunaungurumisha reli ya kisasa'' - Majaliwa

Jumanne , 20th Apr , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, leo Aprili 20, 2021 ametembelea kituo kikuu cha reli ya kisasa ya SGR, Jijini Dar es Salaam na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katikati wakati wa ukaguzi wa mradi wa SGR

Amekagua jengo kuu ambalo linaitwa Tanzania House ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 100, litatumika kwa abiria na wafanyabiashara.

 Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema, ''kufikia mwezi wa Nane tunatarajia kuanza kuungurumisha reli ya kisasa na niwahakikishie watanzania miradi yote iliyoanzishwa itatekelezeka. Mfumo wetu ni ule ule watumishi wakienda tofauti tunakemea hapo hapo.

Jengo la abiria Tanzania House 

Aidha Majaliwa ameongeza kuwa hana mashaka na mkandarasi wa mradi huo ambaye ni kampuni ya Yapi Merkezi na anaamini anajenga mradi huo kwa kiwango cha juu sana.