Alhamisi , 24th Mei , 2018

Rais wa Marekani Donald Trump ameufuta mkutano wa kihistoria kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un uoliopangiwa kufanyika mwezi ujao.

Amesema uamuzi wake umetokana na "ghadhabu kuu na ukali wa wazi" uliokuwa kwenye taarifa ya karibuni ya Korea Kaskazini.

Trump amesema haingekuwa vyema kuendelea na mkutano huo nchini Singapore Juni 12 kama ilivyokuwa imepangwa.

Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zilikuwa zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa.