Waziri wa fedha wa Kenya Henry Rotich
Bajeti hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 2.26 inatarajiwa kufadhiliwa kupitia ukusanyaji wa ushuru na mikopo kutoka kwa washirika wa kimaendeleo ambapo Serikali inalenga kukopa shilingi bilioni 778 hatua ambayo itaongeza deni la kenya ambalo kufikia sasa ni shilingi trilioni 3.32.
Matumizi zaidi itaelekezwa kwa ujenzi wa miundo mbinu ikiwa ni pamoja ujenzi wa reli ya kisasa, kuimarisha usalama, huduma za afya na pia kuziwezesha serikali za majimbo.
Na huko nchini Uganda Makadirio ya bajeti nchi hiyo kwa mwaka 2016 na 2017 iliyosomwa jana ni ya jumla ya dola bilion 7.5 ambayo ni sawa na trillioni 27. 3 pesa za Uganda, tofauti na bajeti ya mwaka uliopita ya mwaka 2015 na 2016 ambayo ilikuwa ni dola bilioni 6.9.
Bajei kubwa mwaka huu nchini Uganda imeelekezwa kwa wizara ya kazi na uchukuzi ambayo ilipewa dola blioni 1.1 huku wizara ya ulinzia ikipewa dola milioni 435. Wizara ya afya imepata dola milioni 525.
Wizara ya nishati na maendeleo ya madini ilipata dola milioni 695 huku Wizara ya kilimo ambayo nidiyo muhimu nchi Uganda ikiewa dola milioni 522.
Nchini Tanzania Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango jana akiwasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo bajeti nzima ya mwaka huu ni shilingi trilioni 29.539, ambapo bajeti ya maendeleo imeongezwa mpaka kufikia asilimia 40 kwa mara ya kwanza Tanzania.