Jumamosi , 19th Mei , 2018

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imepokea msaada kutoka Jamhuri ya Watu wa China wa Bilioni 146.47 kwa ajili ya ujenzi wa chuo Kikuu cha usafiri pamoja na kuendeleza ujenzi wa reli ya standard Gauge ambayo umeanza hivi sasa.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Mhe. wang Ke wakibadilishana mikataba baada ya kuitia saini makubaliano

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James mara baada ya ghafla ya kutia saini ya mkataba wa msaada wa kifedha na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Mhe. Wang Ke uliofanyikia Ofisi za Hazina Jijini Dar es salaam leo Mei 19, 2018 na kusema uwamuzi huo umefikiwa baada ya China kuona inaombwa msaada mara kwa mara.

"Serikali ya China baada ya kuona mara nyingi tunaiomba msaada wa kutusaidia ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard Gauge sasa wameona kwa utashi wao kuisaidia serikali yetu ambapo wao utaratibu wao wanaanza na upembuzi wa awali na yakinifu ambazo zitagharimu shilingi bilioni 3.22 nazo zitafadhiriwa na China maana ni kama msaada", amesema Doto.

Mtazame hapa chini Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akielezea zaidi..