Alhamisi , 26th Jan , 2023

Jeshi la Polisi nchin limeanza kuifanyia kazi taarifa ya tahadhari iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani kwamba kuna uwezekano wa kutokea uhalifu wa kigaidi katika maeneo yanayopendwa kutembelewa na watu wengi wakiwemo wageni hapa nchini.

Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime,

Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime, amesema kuwa licha ya tahadhari hiyo lakini hali ya ulinzi na usalama hapa nchini  ni shwari na kwamba matukio makubwa yanayoweza kuleta hofu kwa wananchi yanaendelea kudhibitiwa.

Taarifa iliyotolewa jana Januari 25, 2023 na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania 

Aidha SACP Misime amesema kwamba pale itakapobainika uwepo wa jambo au watu wenye kutia shaka kutokana na mienendo yao  taarifa zitolewe haraka ili ziweze kufanyiwa kazi.