Alhamisi , 8th Dec , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba wala halichukii hata kidogo jina alilopewa la 'Bi tozo' na kwamba serikali itaendelea kutoza kodi na tozo kwa lengo la kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 8, 2022, wakati akihitimisha mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa uliofanyika mkoani Dodoma.

"Serikali yetu haina mashine ya kurudufua fedha uchapaji wa fedha una kanuni na sheria zake, kikubwa tunachoweza kufanya ni kudhibiti uchumi, fedha yetu isishuke na isitoke nje, lakini ili tuweze kutekeleza mipango yetu ya maendeleo ni lazima tukusanye kodi, lazima tukalipe tozo, lazima tuwekeane tozo na wala sichukii lile jina mlilonipa la Bi tozo, lakini ninapohisi hapa panahitaji mchango wa wananchi ili hili liende sitasita kufanya hivyo," amesema Rais Samia