
Jenista Mhagama - Wazir anayehusika na sera
Muswada ambao unaonekana kuwabana wanufaika wa mikopo hiyo ya elimu ya juu ambapo inaonesha kuwa mnufaika aliyejiajiri atalipa kiasi kisichopungua laki moja na elfu 20 au asilimia 15 ya kipato chake.
Kwa mujibu wa muswada huo kwenye sheria ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu waajiri wanaoshindwa kuwasilisha marejesho ya mwezi baada makato wataadhibiwa ambapo mwajiri atawajibika kuitaarifu bodi wafanyakazi wake wote ambao wamesoma kwa mkopo.
Aidha katika Muswada huo taasisi za umma, bodi,wakala, na tume zimebanwa zirekebishe au kuwianisha mishahara, posho na marupurupu kwa watumishi wake.
Kwa upande wa mrekebisho ya sheria ya leseni na usafirishaji, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini,(SUMATRA), kutaongezwa kifungu ili kuweka masharti kwa mkosaji kulipa faini pindi anapokubali kosa baada kufuata taratibu za mahakama.