Alhamisi , 24th Mei , 2018

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani ikiwemo kutofautisha faini wanatozwa waendesha pikipiki kuwa tofauti na zile zinapigwa za mabasi ya abiria na magari mengine tofauti ya usafirishaji.

Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa wakati mwingine ajali za kizembe zinatokea kwa waendesha bodaboda kutokana na kukimbia kutozwa faini kubwa kuliko wa uhalisia wa vyombo wanavyoviendesha.

"Lengo za faini hizo zitakua ni kwa ajili ya kutoa onyo kwa waendesha vyombo hivyo vya moto ambao takwimu zinaonyesha kwa sasa ndio wanasababisha ajali nyingi zaidi ambazo zinapelekea madhara kwa binadamu lakini pia wengi kuacha pikipiki vituo vya polisi kutokana na kushindwa kulipa faini hizo", amesema Mwigulu.

Msikilize hapa chini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akielezea zaidi.