Alhamisi , 26th Mei , 2022

Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Profesa Jamal Katundu ametangaza kiwango kipya cha kikokotoo cha mafao ya mkupuo ambapo sasa ni asilimia 33 kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii.

Amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano kati ya Serikali, Chama cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) bada ya kusitishwa kwa kanuni zilizotengenezwa Desemba 28 mwaka 2018.