Ijumaa , 11th Aug , 2017

Serikali imetaifaisha magari matatu ya kifahari kati ya saba yaliyokutwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye makontena, alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini na kubainika hayakuwa na Nyaraka stahiki.

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Biswalo Mganga.

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Biswalo Mganga amesema kuwa Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imeamuru washtakiwa wa magari hayo Sulatani Ibrahimu rai wa Uganda na Ramadhani Ukwaju wa Tanzania kulipa faini.

Kati ya Makosa wanaoyoshatikiwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na udanganyifu kwa m aafisa forodha kuhusu vitu walivyokuwa wameviingiza nchini ambapo nyaraka zao walionyesha walikuwa wameingiza viatu na nguo za mitmba lakini kwenye makontena kulikua na magari hayo ya kifahari.

Aidha Kosa lingine wanaoshatikiwa watuhumiwa hao ni pamoja na kusabiashia serikali hasaara zaidi ya milioni tisini kutokana ukwepaji wa kodi kutoka na uingizaji huo wa magari ya thamani kwa kulipa ushuru kidogo wa nguo na viatu.