Jumatatu , 17th Jul , 2017

Serikali imeahidi kupambana na kwa kufanya msako wa usiku na mchana kuhakikisha watu wanaochimba na kuchota mchanga sehemu ambazo haziruhusiwi wanachukuliwa  hatua kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina

Hayo yamesemwa leo mapema na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina ambapo amesitisha shughuli za uchimbaji na uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo mbalimbali yasiyo rasmi jijini Dar es salaam ili kuweza kuondokana na tatizo la uchafuzi wa mazingira.

Wakati wa ziara ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju amesema kuwa kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika kwa urahisi, manispaa zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na ili kubaini kama kuna uwezekano wakuchimba mchanga.

Aidha, amesema kuwa ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa kuandaa utaratibu mfupi wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Halmashauri pamoja na NEMC

“Halmashauri zote zilizo na eneo ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufuata taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”amesema Mpina