Jumatano , 21st Sep , 2022

Serikali ya Tanzania inatarajia kufanya marekebisho kadhaa katika tozo za miamala ya kifedha ikiwani pamoja na kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu na kufuta tozo za kuhamisha fedha ndani ya benki moja, ili kuepuka utozaji kodi mara mbili.

Kamishna Msaidizi wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, William Mhoja

Hayo yamebainishwa leo na Kamishna Msaidizi wa  Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, William Mhoja wakati akitoa ufafanuzi kufuatia kauli ya Waziri wa fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali katika miamala hiyo.

Mhoja amesema kuwa serikali inakusudia pia kusamehe tozo za miamala kuanzia Shilingi 0 hadi 30,000 kwa huduma zote za miamala ya fedha ambapo vyote vitawekwa bayana kwenye kanuni baada yakukamilika na kuanza kutumika Oktoba 1, 2022.