Ijumaa , 20th Mei , 2022

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Patrobas Katambi amesema Serikali inakwenda kwenye hatua ya kufanya ukaguzi kuona kama fedha zilizotengwa na serikali kwajili ya walemavu zinawafikia ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini ya kujua fedha hizo zinawafikia

Naibu waziri Patrobas Katambi ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa chuo cha ufundi stadi na marekebisho cha Masiwani Jijini Tanga. 

Amesema Halmashauri zote nchini zinaendelea kuelekezwa kwamba katika makusanyo ya fedha za Halmashauri amesisitiza asilimia 2 iendelee kutolewa kwajili ya walemavu.

 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la NSSF Mashaji Mshombe amesema jukumu la msingi la kutoa na kusaidia jamii katika masuala muhimu kwa maendeleo ya Taifa mojawapo ni elimu,  na afya. 

Mkuu wa chuo cha walemavu Masiwani Joyria Msuya na Mbunge wa viti maalumu Kigoma Zainab Katamba  wameitaka jamii kuwapenda watu wenye ulemavu. 

Maeneo ambayo yamejengwa vyuo vya walemavu  Nchini ni Daresalam,   Tabora,  Singida, Mtwara, Mwanza na Tanga ambapo Mkoa wa Tanga umetumia kiasi cha shilingi milioni 121 kwajili ya  ya kuwawezesha watu wenye ulemavu.