Jumanne , 16th Nov , 2021

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji, amesema wizara inasubiri ripoti ya tume iliyoundwa kuchunguza tukio la aliyewahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kuvamia kituo cha utangazaji cha Clouds mwezi Machi 2017.

Aliyewahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari hii leo Novemba 16, 2021, baada ya kuwasilisha taarifa ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru Dkt Kijaji amesema tume ilishakamilisha uchunguzi wake hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni tume hiyo kuikabidhi ripoti yake kwa wizara.