Ijumaa , 15th Oct , 2021

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, pamoja na wenzake wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha.

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya

Hukumu hiyo imetolewa leo Oktoba 15, 2021, na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha, Odira Amworo.

Wengine waliohukumiwa katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu na Daniel Mbura.