Jumamosi , 3rd Dec , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha zinatekeleza miradi ya maendeleo kwa ubora na kuzingatia matumizi sahihi ya fedha za umma na kuahidi kuwa ataendelea kufuatilia bila kuchoka.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na wanafunzi Sumbawanga

Sendiga ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi vyumba  Hamsini (50) vya madarasa kwenye shule za sekondari za Manispaa ya Sumbawanga, mradi  unaolenga kuongeza madarasa kwa ajili ya mapokezi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.

Mgawanyo wa vyumba vya madarasa hayo kwa kila halmashauri ni Manispaa ya Sumbawanga (56), Nkasi (26 ), Kalambo (63) na Sumbawanga DC (46) na kuwa madarasa hayo yatakamilika Desemba 15 mwaka huu.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Justin Malisawa alitoa wito kwa wazazi na walezi kujiandaa kuwapeleka shule watoto wao kwani serikali imeweka miundombinu karibu na maeneo yao na kuwa hakuna tena kikwazo kuhusu uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye shule za msingi na sekondari.