RPC azungumzia Ukamataji Lucky Vicent

Thursday , 18th May , 2017

Kaimu Rpc Mkoani Arusha Bw. Yusuph Ilembo amedai kwamba licha ya kuwakamata wamiliki wa shule za binafsi, viongozi wa dini pamoja na Meya wa Arusha kwa kufanya mkutano pasipo kibali maalumu, ameeleza sababu nyingine ilikuwa ni kutoa ulinzi.

Akifanya mahojiano na Muandishi wa East Afri radio, mmoja kati ya waandishi waliopata shuruba ya kukamatwa na kuachiliwa, Bi Janeth amesema kuwa Kwa mujibu wa Kaimu RPC mkoni hapo amedai kuwa watu hao wanashikiliwa kwa kuwa walikuwa na kiasi kikubwa cha fedha hivyo isingekuwa salama kama wasingepatiwa usalama.

Aidha Janet ambaye ni muandishi wa habari ameongeza kuwa hadi wakati wanaondoka kituoni hapo wamewaacha Meya Kalist Lazaro, Wamiliki wa shule binasi viongozi wa dini wakiwa chini ya ulinzi wakifanyiwa mahojiano.

Sikiliza hapa chini mahojiano hayo.