Jumatano , 18th Mei , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema kwa Sasa Mkoa upo shwari kufuatia Operesheni kabambe ya kuwakamata Panya road waliokuwa wakifanya matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla

RC Makalla amesema mpaka Sasa Operesheni imefanikiwa kuwafikisha Mahakama Watuhumiwa 35 na wengine 17 wanaendelea kufanyiwa Uchunguzi.

"Nitoe tu rai kwa wenye nia ovu ya kuchafua amani ya mkoa huu wasahau tuko timamu kuhakikisha kwamba tunafanya kazi usiku na mchana, niwapongeze sana Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam" amesema Makalla

RC Makalla amewatoa hofu Wananchi wa mkoa huo na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kuvunja Uti wa mgongo wa mtandao mzima wa Panya road.

Ili kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii mara kwa mara, RC Makalla amesema wameweka Mpango mkakati endelevu kwa kudhibiti uhalifu wa aina yoyote usitokee kwenye mkoa huo