Ijumaa , 25th Mei , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameyaomba mashirika binafsi kuona umuhimu wa kuwawezesha wafungwa wanaotoka magerezani kupitia mpango wa 'Parole' ili wafungwa waweze kupata kianzio cha maisha wanaporudi uraiani kuendelea na maisha yao.

Mh. Wangabo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Parole Mkoa wa Rukwa ambayo hudumu kwa miaka mitatu .

Amesema kuwa wafungwa wengi wanaotoka kwa mpango huo wanakuwa wametumikia kifungo cha zaidi ya miaka minne gerezani na watokapo huwa na ujuzi wa kuweza kujiajiri na kuweza kuendelea kulitumikia taifa katika kukuza uchumi na kuacha kuwa tegemezi katika familia.

Pamoja na hayo Mkuu wa Magereza   Mkoa wa Rukwa ACP. Simon  Ihunja amezitaja changamoto zinazowakumba wafungwa hao wanapotoka gerezani  ni kukosa kuwezeshwa baada ya kutumikia vifungo vyao.