Jumapili , 10th Oct , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaonya viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia Mawaziri hadi Wakurugenzi kutumia vizuri fedha za mkopo jumla ya Shilingi Trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Onyo hilo amelitoa leo Jumapili Oktoba 10, 2021 wakati akihutubia taifa kupitia uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

''Kwa wale wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi, mkinitazama hivi mnasema Mhe. Rais ni mweupe lakini nina rangi halisi, kwahiyo wanaotaka kuzijua rangi zangu halisi wajaribu kudokoa pesa hizi au wabadilishe matumizi ya fedha hizi bila maelewano,''amesema Rais Samia.

Tazama Video hapo chini akieleza zaidi