Ijumaa , 7th Mei , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema anatamani kuwalipa wazee wote hata shilingi elfu 30 kwa mwezi lakini hali ya uchumi inamkwamisha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Amesema hayo leo Mei 7, 2021 alipoongea na wazee wa Dar es salaam katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

''Suala la wazee wote kuwalipa pensheni tulianza kulijadili serikalini tangu mwaka 2014 tukaona mzigo ni mkubwa sana, tukaenda angalau kuanzia miaka 70 bado mzigo ukawa ni mkubwa, sitaki kuwadanganya wazee wangu'' - Rais Samia Suluhu.

''Natamani sana ningewalipa hata pensheni ya elfu 30, ila kwa hali ilivyosasa, hali ya uchumi wetu Tanzania tumeshuka kutoka asilimia 7 mpaka 4.7 kutokana na janga la Corona, naomba mnipe muda niangalie uchumi wetu unaendaje'' - Rais Samia Suluhu.

Aidha suala la wazee kuwa na uwakilishi bungeni Rais Samia amesema, ''Suala la uwakilishi bungeni na kwenye mabaraza mengine ni la muhimu sana, lakini nikishukuru chama changu cha CCM kimetambua kundi la wazee na wazee wanawakilishwa vizuri kupitia nafasi ya umoja wa wazazi''.

''Lakini kwasababu mmezunguma nami ila kwa bahati mbaya tumamemaliza nafasi za uteuzi kwa kipindi hiki ila mbeleni huko kujako tutalizingatia hili'' - Rais Samia.