Rais Magufuli atuma rambirambi kwa Mufti

Tuesday , 19th Sep , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Septemba 19 ametoa rambirambi kwa Mufti wa Tanzania Shekhe Aboubakar Zubeir kufuatia msiba wa kaka yake Shekhe Saad Zubeir Ally.

Rambirambi hiyo imekabidhiwa na mwakilishi wa Mh. Rais Kanali Mkeremy alipofika msibani Kinondoni. Msiba huo pia umehudhuriwa na Shekhe wa mkoa wa Dar es salaam  Alhad Mussa Salum.

Kanali Mkeremy amewasilisha rambirambi hiyo kwa niaba ya Mh. Rais na kupokelewa na Shekhe Aboubakar Zubeir nyumbani kwake Kinondoni mtaa wa Ufipa ambapo ndio msiba ulipo. Shekhe Saad Zubeir Ally alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkut