Rais Magufuli afanya uteuzi

Thursday , 11th Jan , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Januari 11, 2018 amefanya uteuzi na kuwateua Bw. Alphayo Kidata pamoja na Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi kuwa mabalozi wa nchi. 

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Alphayo Kidata umeanza tarehe 10 Januari, 2018 na kabla ya uteuzi huo, Bw. Alphayo Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amesema kuwa Mabalozi Mabalozi hao wateule watapangiwa vituo vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika.

Recent Posts

Mwanafunzi Aqulina Akwilini Baftaha aliyeuawa na poilisi

Current Affairs
CCM yatoa kauli yake kuhusu kifo cha mwanafunzi