Polisi wampiga risasi mke wa Mwenyekiti

Wednesday , 9th Aug , 2017

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limemfyatulia risasi ya mguuni mke wa Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mabatini majengo mapya usiku wa kuamkia leo.

Majeruhi huyo ametambulika kwa jina la Editha Ntobi ambapo baada ya kufyatuliwa risasi hiyo alivuja damu nyingi na kupelekea kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambapo amelazwa.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi na kusema uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea kufanywa ili kubaini ni kitu gani kilikuwa chanzo cha tukio hilo.