Jumanne , 16th Nov , 2021

Idadi kubwa ya Polisi waliojeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea hii leo nchini Uganda karibu na Kituo Kikuu cha Polisi cha nchi hiyo wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mulago nchini humo.

Baadhi ya majeruhi waliotokana na milipuko nchini Uganda

Mlipuko huo umetokea hii leo Novemba 16, 2021, katika maeneo tofauti ya barabara ya Bunge na Kituo Kikuu cha Polisi Kampala, na kusababisha majeruhi kadhaa.

Ambapo kwa mujibu wa kituo cha Television cha Uganda cha NTV kimeeleza kuwa hadi sasa majeruhi 27 wanapata matibabu katika hospitali ya Mulago.