PF3 kuendelea kama kawaida - Polisi

Thursday , 18th May , 2017

Masaa kadhaa baada ya Waziri Mwigulu Nchemba kutoa maamuzi ya majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata, kuwa wanapaswa kupewa matibabu kwanza wakati wakifuatilia PF3. Jeshi la polisi limeibuka na kutoa ufafanuzi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba-ACP

"Fomu ya Polisi namba 3 ijulikanayo kama PF.3 hutolewa kwa mtu baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji au muathirika kwa matukio yenye madhara mwilini, ajali au matukio yenye kuleta mashaka kuhusu vyanzo vyake kama vile kipigo, kujeruhi, ubakaji, kulawiti,  kunywa sumu na mengineyo. Ieleweke wazi kwamba matumizi ya PF3 ni ya lazima na yanaendelea kama kawaida  kwa mujibu wa sheria" alisema Advera Bulimba