Alhamisi , 26th Mei , 2022

Asasi ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA) imesema kuwa Sakata linaloendelea ndani ya chama cha NCCR Mageuzi , suluhu yake ni viongozi waliokaa madarakani muda mrefu kuanzisha ushindani wa haki kwenye viti hivyo ili kuwepo na Demokrasia ndani ya vyama vyao.

Mkurugenzi wa Asasi ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA) Thomas Ngawaiya

Mkurugenzi wa Asasi hiyo Thomas Ngawaiya amewashauri NCCR - Mageuzi wakae na kushauriana ili kutafuta suluhu ya mgogoro huo 

‘’Nawaambia hawa wapinzani kwamba inapofika wakati, kwanza  wengine wamefika mpaka wamekua wazee sana, naomba demokrasia iwepo, wenzako wakichaguliwa ama wewe ukiambiwa unaendelea basi endelea, mimi nilikua nafikiri NCCR wakae, washauriane, wajadili, mara sasa wanaanza kwenda mahakamani, jambo hili halipendezi’’