Jumanne , 7th Jan , 2020

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile, amemuagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt Atupele Mwandiga, kuhakikisha anapata taarifa ya utoaji wa dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.

Naibu Waqziri Ndugulile akisalimiana na

 

Agizo hilo limekuja wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo, alipotembelea hospitali hiyo kujionea utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na kushuhudia mmoja wa mama aliyejifungua hospitalini hapo, kupewa dawa mara moja badala ya mara tatu kama iilivyoandikwa na Daktari.

Dkt Ndugulile amesema kuwa amekasirishwa na utendaji kazi wa manesi katika wodi ya mama na mtoto kwa kutozingatia utoaji huduma, hasa kuhakikisha wazazi na watoto wanapewa dawa kwa wakati na kwa idadi sahihi.

Ameongeza kuwa lengo la mgonjwa kupewa huduma ni kuhakikisha anapona na sio kufanya aendelee kupata tabu.

"Haiwezekani mgonjwa kanunua dawa zake kwa fedha zake lakini bado hata hamzingatii kumpatia dawa mnategemea ataponaje” amesema Dkt Ndugulile.

Aidha Dkt Ndugulile ameutaka uongozi wa hospitali hiyo, kuhakikisha wanaratibu utoaji wa huduma hospitalini hapo ili kuepukana na malalamiko ya wagonjwa na kupoteza imani ya wananchi kwa hospitali hiyo.