Jumamosi , 19th Mei , 2018

Kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na kampuni ya EATV LTD yenye lengo la kuwasaidia watoto wa kike wanapokuwa katika kipindi cha hedhi imewafikia wanafunzi wa shule ya sekondari Buza.

Akiwasilisha msaada huo Afisa Masoko wa EATV LTD Basilisa Biseko amesema kuwa lengo la Kampeni hiyo ni kumsaidia mtoto wa kike kuondokana na tatizo la kushindwa kuhudhuria shuleni wakati wa kipindi cha hedhi.

“Namthamini imekuja ili kusaidia kuondokana na tatizo la mabinti wengi wa kitanzania kutohudhuria vipindi mashuleni pindi wanapokuwa kwenye hedhi kutokana na kukosa taulo za kike”, amesema Basilisa.

       Mbunge wa Temeke Mh. Abdallah Mtolea akigawa taulo za kike kwa mabinti wa Sekondari ya Buza.

Kwa upande wake Mbunge wa Temeke Mh. Abdallah Mtolea ameishukuru EATV kwa kutambua na kuthamini mchango wa mtoto wa kike katika Jamii na kuahidi kuwa ataungana nao katika kufanikisha kampeni hiyo miaka yote.

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Buza Bi. Ruthbetha Magomi amesema kuwa elimu kuwa msaada huo kwa shule yake utasaidia kunufaisha mabinti wengi ambao wanapata changamoto pindi wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi.