Alhamisi , 11th Aug , 2022

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limemkamata mtuhumiwa maarufu wa wizi wa pikipiki anayefahamika kwa jina la Laurenti Lazaro (61) Mkazi wa  Kanoge Wilaya ya Mpanda akiwa ameiba  pikipiki tano za watu tofauti tofauti

Kamanda wa Polisi Katavi Ali Hamad Makame, amesema kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi  waliandaa msako mkali  wa kupambana na uhalifu  na waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo  akiwa na pikipiki ya wizi yenye Namba za usajiri   MC  915 CDV   aina ya  HONLG yenye rangi nyekundu.

Kamanda  Makame amesema  baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa  na kufanyiwa mahojiano  ya kina  amekiri kuwa aliiba pikipiki  nyingine nne  kwenye maeneo tofauti tofauti ya Mkoa wa Katavi  na aliweza kwenda kuzionesha pikipiki hizo.

Makame ameeleza kuwa mtuhumiwa  huyo alikuwa akiiba kwa kutumia mbinu ya kutembea na funguo  bandia ambazo  ndizo alikuwa  akizitumia  kuibia pikipiki zinazokuwa zimepakiwa  kwenye maeneo mbalimbali  na wamiliki wa pikipiki hizo.