Jumamosi , 8th Mei , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amempa gari Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kama zawadi ya kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ambapo hii leo Mei, 8, 2021, ametimiza umri wa miaka 96.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi gari aliyompa kama zawadi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Awali kabla ya kumkabidhi gari hilo, Rais Samia, alisema kuwa ameamua kumpa zawadi hiyo ili kumuondolea kadhia ya kupanda na kushuka gari lake analolitumia kwa sababu hivyo ameamua kumpa gari la chini ili awe anapanda na kushuka kwa uzuri zaidi.

"Kama mnavyojua leo ni siku ya kuzaliwa kwa Mzee wetu na siku hii waalikwa hutoa zawadi kwa mzaliwa na nimemuangalia na kimo chake na usumbufu anaoupata wakati wa kupanda na kushuka gari tulilompa, serikali tumeona tumpunguzie kadhia hiyo hivyo tutampatia Benz ya chini gari itakayompa raha", amesema Rais Samia