Jumanne , 21st Jun , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linaendelea na uchunguzi juu ya tukio la mauaji ya Johnson Thomas 14, mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Buhalahala iliyopo halmashauri ya mji Geita ambaye mwili wake uliokotwa pembeni ya mto siku sita baada ya kupotea.

Ndugu na majirani wa familia hiyo wanasema siku ya mwisho mtoto huyo alitoka nyumbani majira ya saa11 jioni  kwa ajili ya kupeleka nguo za shule kwa fundi lakini tangu hapo hakuonekana mpaka mwili wake ulipookotwa ukiwa umetobolewa jicho na kusagwa unyayo.

Kutokana na matukio ya ukatili kwa Watoto kuongezeka mkoani humo Baadhi ya wanafunzi wenzie na marehemu wameiomba serikali kuwawekea mazingira rafiki kwa ajili ya usalama wao.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe anasema jeshi bado linaendelea na uchugnguzi juu ya tukio hilo linalohusisha imani za kishirikina.