Jumatatu , 3rd Jan , 2022

Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga imesema kwamba tayari imeshatenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuboresha vivutio vilivyomo mkoani Ruvuma, ikiwemo bustani pekee ya wanyama ya Ruhila ambayo ipo katikati ya mji wa Songea.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro

Akizungumza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damas Ndumbaro, amesema kwamba mbali na bustani hiyo pia wizara itaboresha pia msitu wa Matogoro ambao mapango yake mawili yanatumika kama rufaa ya matibabu ya jadi kwa wagonjwa wanaofika hapo.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema kwamba tayari bajeti ya kutengeneza barabara ya kufika katika msitu wa Matogoro ambapo kuna mapango yanayotumika kama rufaa ya wagonjwa iko tayari na mkandarasi anatarajiwa kuanza kazi.