Jumatano , 17th Aug , 2022

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Hamad Masauni amesema serikali inaangalia namna ya kutafuta ufumbuzi wa kutatua tatizo la kimpaka kwenye bahari ya Hindi kati ya Tanzania na Kenya baada ya kuwepo kwa muingiliano wa shughuli za uvuvi kati ya wavuvi wa nchi hizo mbili 

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Hamad Masauni

 

Waziri Masauni ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea bandari ndogo ya Moa na baadae Horohoro kwenye  mpaka wa Tanzania na Kenya. 

Amesema kuwa  kati ya mambo ambayo serikali inataka kuanza nayo ni pamoja na kuanzisha kitengo cha uhamiaji cha wanamaji kitakachosaidia pindi kikosi maalumu cha kuzuia magendo Zanzibar KMK watakapoondoka wilayani humo kazi ya kulinda mipaka na usalama ifanywe na jeshi hilo la uhamiaji.

 
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanal Maulid Sulumbu amekiri ukosefu wa kituo cha polisi katika eneo kuimarisha masuala ya ulinzi kutokana na eneo hilo kuwa lango la wahamiaji haramu. 

Ziara ya Waziri Masauni imekuja siku moja mara baada ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutembelea katika wilaya hiyo ambapo alikutana na kero ya wahamiaji haramu wanaopitia mpaka wa Horohoro