Jumatano , 23rd Jun , 2021

Mbunge wa Viti Maalum Neema Lugangira, ametoa pendekezo kwa serikali kuhusu faini ya bodaboda na bajaji kwamba waweke mifumo kwenye leseni za madereva hao utakaoruhusu dereva kulipa faini kwa makosa mawili pekee na akitenda kosa la tatu basi afungiwe leseni yake.

Mbunge wa Viti Maalum Neema Lugangira

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 23, 2021, wakati akitoa mchango wake katika muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2021, na kuongeza kuwa serikali isiache faini ya shilingi 10,000 pekee kwa bodaboda ama madereva bajaji bali iweke na mfumo wa kuwawajibisha huku lengo likiwa ni kulinda maisha ya watumiaji wa usafiri huo pamoja na bodaboda wenyewe.

"Kuhusu faini za bodaboda ningependa kupendekeza kwa serikali ije na mfumo wa kuweka 'point system' kwenye hizi leseni kwamba huyu mwendesha bodaboda au bajaji akifanya kosa la kwanza na la pili alipe 10,000, akifanya kosa la tatu kulingana na ile point system leseni yake ifungiwe kwa kufanya hivyo tutalinda watumiaji wa zile pikipiki na maisha yao wenyewe tusiache hii faini ya elfu 10 pekee yake,"amesema Mhe. Neema Lugangira