Ijumaa , 24th Jun , 2022

bunge wa jimbo la Enugu nchini Nigeria, Ike Ekweremadu na mkewe, Beatrice Nwanneka Ekweremadu wamefikishwa mahakamani katika jji la London, Uingereza kwa tuhuma za kumsafirisha kijana wa mtaani kutoka Nigeria mpaka Uingereza kwa ajili ya kwenda kumtoa figo.

Ike Ekweremadu

Walimsafirisha kijana wa miaka 15 kutoka mtaani kwa lengo la kwenda kuchangia figo kwa binti yao ambaye amelazwa hospital kwa matatizo ya figo, na walimpa ahadi za kwenda kumpa maisha mazuri nchini Uingereza bila kumwambia atahitajika kutoa figo.

Zoezi hilo halikufanikiwa hospitali baada ya kugundulika walifanya udanganyifu kwa kijana huyo ambaye hakuwa tayari kutoa figo na waligushi pasipoti inayoonesha ana umri wa miaka 21.