Jumamosi , 26th Mei , 2018

Mbunge wa jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma kupitia CHADEMA, Mh. Kasuku Samson Bilago amefariki dunia mchana huu akiwa katika Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, ambapo ameeleza kuwa taarifa zaidi juu ya msiba huo zitatolewa muda si mrefu.

Mheshimiwa Bilago pia alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA.