Ijumaa , 13th Mei , 2022

Mbunge wa jimbo la Sengerema Hamis Tabasamu, ameishauri Wizara ya Maji kutenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 ili iweze kununua helikopta itakayotumika kwenye ukaguzi wa miradi ya maji nchini badala ya kutumia magari kwani yanachosha.

Mbunge wa jimbo la Sengerema Hamis Tabasamu

Kauli hiyo ameitoa bungeni hii leo Mei 13, 2022, wakati akichangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maji iliyosomwa hapo jana na Waziri wake Jumaa Aweso.

"Mh. Aweso ushauri wangu, kwa kutumia magari kutembea nchi nzima unaweza ukachoka kuifikia miradi yote kuikagua, Watanzania wanatakiwa waambiwe kutumia helikopta ni gharama ndogo sana mafuta lita 400 unatoka nayo Dar es Salaam unaweza ukakagua miradi mpaka 10 ukafika Sengerema, mnashindwaje Wizara ya Maji kutoa bilioni 1.5 mkanunua helikopta,"amesema Mbunge Tabasamu