Alhamisi , 26th Mei , 2022

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma amesema katika uongozi wa awamu ya Sita wa Rais Samia Suluhu Hassan sio wanawake tu wanaofurahia bali hata wanaume wanafurahia uongozi wake

Musukuma ametoa kauli hiyo leo Mei 26 bungeni Jijini Dodoma wakati wa kuchangia azimio la kumpongeza Rais Samia kwa uongozi wake 

""Kwa uongozi wa Mama Samia sio wanawake tu wanaomfuraia hata sisi wanaume tunamfuraia sana, hata vyama vya upinzani, hebu angalia leo Mbowe ndiye anaongoza kwenda Ikulu najua alipamisi sana lakini amepata nafasi yakuingia na kutoka zaidi ya mara tano"

Musukuma amesema baada ya kuondokewa na Rais wa awamu ya tano, Tanzania imepata kiongozi ambaye ameenda kuionyesha Afrika kwamba Tanzania ni nchi ambayo inadumisha amani.

Leo Bunge la Tanzania limepitisha azimio la la kumpongeza Rais Samia Suluhu baada ya kupokea Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) na kwa kutambuliwa kama miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa duniani