Jumamosi , 15th Mei , 2021

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021, zenye kauli mbiu isemayo TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu, itumie kwa usahihi na uwajibikaji, zitahitimishwa Oktoba 14, 2021, wilayani Chato mkoani Geita.

Mwenge wa Uhuru

Taarifa hiyo imetolewa Visiwani Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, Mei 17 mwaka huu anatarajiwa kuzindua mbio hizo kitaifa katika uwanja wa Mwehe, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja.

Ambapo baada ya uzinduzi huo Mwenge wa Uhuru utaanza mbio zake chini ya vijana shupavu sita kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ), kwa siku 150.