Ijumaa , 12th Aug , 2022

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kamishina msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amekagua mazoezi maalum ya kikosi cha mbwa na farasi ambao wanatumiwa na Jeshi hilo kuwatambua wahalifu mbalimbali wakiwemo wamadawa ya kulevya, silaha pamoja na mabomu

Amesema kuwa kupitia kikosi hicho wamejipanga vyema kukabiliana na madawa ya kulevya pamoja na vilipuzi vya aina yeyote ile katika mkoa wa huo

Sambamba na hilo kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo kupitia kikosi cha mbwa na farasi kinatoa mafunzo kwa mbwa wa kirai ilikuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa wa Arusha

Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha Mbwa na farasi mkoa wa Arusha mrakibu msaidizi wa Polisi ASP William Mwaisumo amesema kuwa kikosi hicho kimejipanga vyema kutoa mafunzo kwa mbwa wote watao letwa kupata mafunzo ya ulinzi na utambuzi wa madawa vilipuzi.