Jumamosi , 1st Oct , 2016

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imesema kwamba kitendo cha Urusi kuongeza mashambulizi nchini Syria kunawalazimisha wapinzani wa lengo wa kati nchini humo kuangukia katika mikono ya makundi ya mlengo mkali.

Msemji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Marekani Mark Toner amesema kuongezeka kwa mashambulizi ya anga yanayofanywa na Urusi na Syria yamefanya hali kuwa ngumu na ya kuchanganya.

Msemaji huyo amesema Marekani huenda ikasitissha ushirikiano na Urusi dhidi ya hatua yake nchini Syria. Lakini Urusi imeishutumu Maekani kwa kujaribu kuliweka kando kundi la Kijihad kwa kutaka kumuondoa madarakani Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema Marekani imevunja ahadi yake yaa kujitenga na kundi lenye nguvu la Jabhat Fateh al-Sham lililkuwa likitambulika huko nyuma kama al-Nusra Front na makundi mengine ya mlengo wa kati.

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imesema kwamba kwa Urusi kuongeza mashambulizi nchini Syria kunawalazimisha wapinzani wa lengo wa kati nchini humo kuangukia katika mikono ya makundi ya mlengo mkali.

Msemji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Marekani Mark Toner amesema kuongezeka kwa mashambulizi ya anga yanayofanywa na Urusi na Syria yamefanya hali kuwa ngumu na ya kuchanganya.

Msemaji huyo amesema Marekani huenda ikasitisgha ushirikiano na Urusi dhidi ya hatua yake nchini Syria. Lakini Urusi imeishutumu Maekani kwa kujaribu kuliweka kando kundi la Kijihad kwa kutaka kumuondoa madarakani rais wa Syria Bashar al-Assad.