Jumanne , 17th Mei , 2022

Rais  Joe Biden ameripotiwa kuamuru kurejeshwa kwa mamia ya majeshi ya Marekani nchini   Somalia.
Rais aliyepita Donald Trump aliyaondoa majeshi ya nchi hiyo yapatayo 700 ambayo yalikua yakilinda amani nchini humo.

Mamlaka za kijasusi za Marekani zinasema kuwa al-Shabab wana majeshi yapatayo   10,000 ambapo licha ya kuendeleza mapambano ndani ya Somalia, kuna mipango ya  kuishambulia Marekani .
Miaka miwili iliyopita kundi hilo lilifanya mashambulizi nchini Kenya katika ubalozi wa Marekani.
Haijajulikana ni wageni wanajeshi wangapi ambao Rais  Biden ameamuru wapelekwe   Somalia.