Jumapili , 2nd Oct , 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba SALVADOR ANTONIO VALDES MESA amewasili jioni ya leo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.

SALVADOR ANTONIO VALDES MESA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba SALVADOR ANTONIO VALDES MESA atafanya ziara ya kikazi ya siku 3 hapa nchini na lengo la ziara hiyo ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya, utamaduni,michezo,kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.

Tarehe 3/09/2016 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba atakutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba SALVADOR ANTONIO VALDES MESA pia atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu na baada ya mazungumzo hayo ya faradha viongozi hao watafanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo MBILI.

Nchi nyingine ambazo Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba anazitembelea ni Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo- DRC-,Botwana na Zimbabwe.