Jumamosi , 12th Dec , 2015

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga, imetengua pingamizi la kupinga kupunguziwa gharama za kesi ya uchaguzi kutoka shilingi milioni 15 hadi milioni tisa iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama mjini, James Lembeli

James Lembeli akihutubia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu

Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya shinyanga, imetengua pingamizi la kupinga kupunguziwa gharama za kesi ya uchaguzi kutoka shilingi milioni 15 hadi milioni tisa iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama mjini, James Lembeli, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Hukumu hiyo imetolewa leo na jaji wa mahakama hiyo Jaji Victoria Makani, ikiamuru Lembeli kulipa kiasi hicho cha pesa badala ya milioni 15 kama ilivyoamriwa awali kwa kila mshitakiwa kulipiwa milioni 5.

wanaolalamikiwa na Lembeli ni mbunge Jumanne Kishimba aliyeshinda kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Kahama mjini, msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria mkuu wa serikali kwa kupinga ushindi wa Kishimba kwa madai uchaguzi mkuu haikufanyika kwa haki pamoja na kutawaliwa na vitendo vya rushwa.